Tuesday, August 2, 2016

Amepewa Moyo Na Mapafu Yasiyofaa Na Kufariki


Msichana aliyefahamika kwa jina la Jésica Santillán, aliwasili katika hospitali ya Duke University Medical Center Marekani, kutokea nchini Mexico ili kupata matibabu kufuatia kuwa na matatizo ya moyo na mapafu.

Jésica alikuwa ni msichana wa umri wa miaka 17, raia wa Mexico, pengine alikuwa na ndoto nyingi kwa taifa lake na familia kwa ujumla lakini alifariki dunia muda mfupi mara baada ya kufanyiwa upasuaji.

Sababu ya kifo chake ilitokana na kuhamishiwa moyo na mapafu (heart-lung transplant) kutoka kwa mtu ambaye hafanani naye kundi la damu.

Je, ulishawahi kupatwa na tatizo kama hilo au linalofanana na hilo? Tuambie kupitia kisanduku cha maoni au tuandikie barua pepe kupitia afyaboraherbalclinic@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *