Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

Wednesday, August 10, 2016


Tabia ya mtu inatokana na malezi aliyoyapata kwa kiasi kikubwa toka kwa wazazi,pia toka kwa walimu mashuleni, mafundisho ya dini,na toka kwa watu anaoonana nao na kuchangamana nao kila siku za maisha yake hasa wakati wa umri mdogo. Kulea watoto kulingana na tamaduni zetu katika karne hii ya teknolojia ni changamoto kubwa.

Watoto wa Dijitali ni wale ambao wamezaliwa katika karne hii ambayo teknolojia ya habari na mawasiliano imesomnga mbele sana kiasi ambacho taarifa zimekuwa nyingi kupita uwezo wakuzidadavua. Wazungu wanaita “Information Overload“.

Watoto hawa wa dijitali wanafahamu mambo mengi sana kuliko ambavyo wanatakiwa kufahamu katika umri husika jambo ambalo linaleta changamoto kubwa katika kulea watoto kwa wazazi wa zamani ambao walizaliwa kipindi ambapo teknolojia haikuwa katika kiwango hiki na mfumo wa malezi walioupata unatofautiana sana na wa sasa na pengine haufanyi kazi katika mazingira ya kisasa. Wazazi hawa nimewaita “Wazazi wa Analojia”.

Katika hali hii utakuta mtoto anafahamu mambo mengi tu ambayo wazazi hawayajui,ina maana mzazi anajifunza toka kwa mtoto,hii ina maana gani? Kuna madhara mara mbili

  • Mzazi anakosa kujiamini katika jukumu lake la kumfundisha mtoto kwani anatambua sasa kuwa mtoto ni mjuaji wakati ungine kumzidi,na anaweza kuamua kutofanya hilo jukumu kwa kujua mtoto anafahamu tayari. Wakati mwingine inakuwa si sahihi.

  • Mtoto anatambua baada ya muda kuwa mzazi wake hafahamu mambo mengi na kuwa yeye anafahamu zaidi. Hivyo naye anaacha kuuliza au kutaka kufahamu toka kwa wazazi. Hivyo anaweza akafanya vitu kwa ufahamu wake tu binafsi au kwa kutafuta msaada sehemu nyingine nje na wazazi wake. Na huenda msaada atakao pata ukawa sio sahihi.

Hali hii ni hatari katika ulezi wa watoto katika jamii yetu na ni lazima kuliangalia kwa mapana sana na kuchukua hatua stahiki.



0

Tuesday, August 9, 2016


Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya ‘Treponema pallidum’.

Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.

Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama vile kujifungua kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa, mtoto kupata matatizo wakati wa ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga.

Ugonjwa wa kaswende huathiri zaidi ya mimba milioni moja duniani kote kila mwaka na kuchangia theluthi mbili ya vifo vya watoto wanaozaliwa wakiwa tayari wameshakufa katika nchi za maeneo ya chini ya Jangwa la Sahara.

Asilimia 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende huishia watoto kufariki wakati wa kuzaliwa.

Pia asilimia nyingine 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende husababisha watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu kupata matatizo ya ukuaji, degedege na kuongezeka vifo vya watoto kwa asilimia 50. Kwa mfano,

Taasisi ya kudhibiti Ugonjwa wa UKIMWI nchini Tanzania (Tanzania National AIDS Control Programme) au NACP katika ripoti yake ya utafiti uliofanywa chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini ilitangaza kuwa, maambukizi yote ya kaswende wakati wa ujauzito Tanzania bara kati ya mwaka 2003 hadi 2004 yaliongezeka kwa wastani wa asilimia 6.7 kwa ujumla, kuanzia mkoani Kilimanjaro ambako maambukizi yalikuwa ya asilimia 0.4 hadi mkoani Tabora ambako yalikuwa ya asilimia 32.

Magonjwa ya UKIMWI na kaswende mara nyingi huambatana pamoja ambapo pia ugonjwa wa zinaa wa kaswende huongeza uwezekano wa mtu kupata UKIMWI.

Je, ugonjwa wa kaswende huambukizwa kwa njia gani?


Kama tulivyosema awali, kaswende husababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Miongoni mwa njia za ugonjwa huu nipamoja na ·

Kupitia kujamiiana bila kutumia kinga au ngono zembe na mtu aliyeambukizwa kaswende.

· Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.

· Kuambukizwa kupitia michibuko au mipasuko kwenye ngozi wakati wa kujamiiana au wakati mwingine pale mtu anapogusana na mtu mwenye kaswende ikiwa wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za ngozi zao.

Sio rahisi mtu kutambua kama ana michibuko au la kwenye ngozi kwani mingine huwa midogo sana isipokuwa ile inayoweza kuonekana kwa macho, lakini huweza kuwa njia ya maambukizo.

Dalili na viashiria vya tatizo hili


Dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea aina ya ugonjwa wa kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;

Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis), Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis),  Kaswende iliyojificha (Latent syphilis), Kaswende ya baadaye (Tertiary syphilis. Itaendelea..............

0

Monday, August 8, 2016


Licha ya ladha yake kuwa chungu, mmea wa “Aloe Vera” una faida nyingi kiafya ukitumika kama tiba katika mwili wa binadamu.

Mmea huu umekuwa na majina tofauti tofauti kama ifuatavyo; kwa lugha ya Kiswahili mmea huu huitwa shubiri mwitu, ambapo katika makabila kadhaa mmea huu huitwa majina mbalimbali kulingana na kabila husika.

Wanyaturu huuita ‘mkankiruni’, Wagogo huuita ‘itembwe’ na wahehe huuita ‘Litembwetembwe.’ Mmea huu huwa na umbo linalofanana na mmea wa mkonge au mmea wa mnanasi, ila huu huwa mlaini zaidi.

Majani ya mmea huu yana sehemu mbili, kuna ganda la nje na majimaji ya ndani (jelly). Ganda la nje lina kemikali za kutibu na ule ute wa ndani na lina virutubisho vingi ambavyo husaidia katika kurutubisha kinga za mwili wa binadamu.

Licha ya mmea huu kuwa maarufu duniani kote, umekua ukitumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali kwa binadamu na mifugo.

Mshubiri pori umekua ukitumika pia kwa kutengenezea vipodozi vya aina mbalimbali kwa ajili ya masuala ya urembo. Mmea huu hupatikana sehemu nyingi sana duniani hasa katika nchi zenye joto.

Tafiti zilizofanywa na mtandao wa ‘Mediclinic’ kuhusiana na mmea huu, zinaeleza kuwa mmea huu una uwezo wa kuchochea utengenezwaji wa tishu zenye afya katika mwili wa binadamu.

Imebainika pia kuwa mshubiri huo una uwezo mkubwa wa kufanya mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri na kutuliza matatizo yanayoathiri mfumo wa fahamu.

Mbali na hayo, lakini pia mshubiri “Aloe Vera” ukitumiwa kama tiba husaidia kuondoa sumu mwilini. Mmea huu mara nyingi hutumiwa na kina baba kutibu maradhi ya ngiri (Hernia). Kwa hakika mmea huu una maajabu mengi katika suala zima la tiba.

Naweza nikadiriki kusema, mmea huu ni tunu tuliyotunukiwa wanadamu kutoka kwa Mola wetu kwa ajili ya tiba. Sidhani kama kuna mmea wenye uwezo wa kutibu maradhi mengi namna hii kama ilivyo kwa mshubiri pori.

Haijaishia hapo pia, mshubiri hutumika katika kusaidia kujenga seli mpya katika mwili wa binadamu baada ya kupata majeraha kama vile kujikata, michubuko, majeraha ya moto na hata vidonda vya tumbo.

Aidha, husaidia matatizo ya kutopata haja kubwa, maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo na hata husaidia kutibu matatizo ya ngozi na chunusi.

Mshubiri umekuwa ukitumika kwa wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kwa ajili ya kuongeza kinga za mwili (CD4), na imebainika mmea huu unapotumiwa vizuri, mgonjwa wa UKIMWI hujikuta katika hali nzuri.

Watu wengi wamekuwa wakitumia mmea huu kama tiba ya ugonjwa wa malaria, lakini pia mmea huu umekuwa ukichanganywa katika vipodozi mbalimbali ili kuvipa uwezo maradufu wa kutunza ngozi.

Unaweza kutumia mmea huu kwa kukata majani yake na kuyasaga kwa kutumia ‘blender’au kuyatwanga kwenye kinu, na kisha kuyachanganya na maji ya vuguvugu Chuja maji hayo na ongeza maji mpaka upate maji ya kiasi cha jagi moja.

Kunywa vikombe viwili mpaka vitatu kwa siku, kwa muda wa siku tano mpaka saba. Hii itakusaidia kuongeza kinga ya mwili wako na unaweza kurudia dozi hii kila baada ya miezi mitatu mpaka minne.

Ni vema kutumia tiba za mimea ili kuepuka kemikali zisizo za lazima katika miili yetu kiafya. Tukiangalia, pia tunaweza kuona kuwa hata baadhi ya dawa za hospitalini hutengenezwa kwa kutumia mitishamba na mimea ya asili.

Mbali na mmea wa mshubiri kutumika kama tiba kwa binadamu, mmea huu pia unaweza kutumika kama tiba kwa mifugo kama vile kuku. Kwa mfano, ugonjwa wa vidonda vya kuku ambao kwa kitaalam huitwa ‘coccidiosis’ na ugonjwa wa mdondo ambao pia kitaalam hufahamika kama ‘Newcastle disease’ Hutibka kwa kutumia mshubiri.

Baadhi ya watu wamekuwa wakiipanda mimea hii katika bustani za maua majumbani mwao, bila ya kujua umuhimu, faida na maajabu ya mmea huu.

Ningependa kutoa wito kwa Watanzania kutopuuza matumizi ya mmea huu. Ni vema tukautumia kwa ajili ya kinga na tiba za magonjwa mbalimbli katika miili yetu.
5

Saturday, August 6, 2016


Nini maana kukojoa kitandani?

Hii ni hali ya kukojoa kitandani wakati mtu amelala, tatizo hili linapotokea kwa mtoto wa chini ya miaka sita sio ugonjwa na mara nyingi huisha lenyewe.

Watoto wengine huendelea kukojoa kitandani mpaka umri wa kubalehe na kuvunja ungo. Lakini tatizo hili hupotea anapokua mtu mzima kabisa.

Sababu kwanini mtoto anayeweza kukojoa mwenyewe mchana kuendelea kukojoa wakati amesinzia haileweki , mara nyingi watoto wa kiume hujikojolea sana kuliko wa kike lakini kuna mahusiano ya kurithi tatizo hili yaani kuna uwezekano mkubwa baba wa mtoto au mama alikuaga kikojozi pia kwenye utoto wake.

Kwa watu wazima tatizo la kukojoa kitandani hua ni ugonjwa flani. Mfano wa magonjwa haya ni,

Kisukari (diabetes mellitus):

Ugonjwa huu huambatana na dalili ya kupata kiu sana, njaa kali na kwenda kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku.

Magonjwa ya njia ya mkojo (chronic urinary tract infection):
Hii ni kutokana na kuharibika kwa kibofu cha mkojo ambacho ni muhimu katika kutambua ujazo wa flani wa mkojo ili mtu aende kukojoa hivyo kuugua kwa kibofu husababisha kisifanye kazi vizuri. mfano cystitis

Magonjwa au kuumia kwa mishipa ya fahamu ( structural or infections of nerves):

Mishipa ya fahamu ni muhimu katika kutoa taarifa za ujazo wa mkojo kwenye kibofu. Kibofu kinapofikisha ujazo wa 300mils mpaka 400mils taarifa hutumwa kwenye ubongo, kisha ubongo hurudisha taarifa za kuruhusu mtu akojoe.

Kuharibika kwa mishipa hii ya fahamu husababisha kujikojolea mfano kuvunjika kiuno, kiharusi, magojwa ya akili, multiple sclerosis na alzeheimers disease.

Kuvimba kwa tezi dume (prostate enlargement):

Tezi dume ni kiungo kinachopitiwa katikati na mirija ya mkojo{urethra}, hivyo kuvimba kwake hubana mirija hiyo na kusababisha kukojoa mara kwa mara[incontinence}.

Vipimo ambavyo hupimwa mahospitalini:

Kupima mkojo kuangalia kama kuna shida yeyote ya mfumo huo.

Kupima puru kama tezi dume imevimba.{digital rectal examination}

X-ray kuangalia kama kuna tatizo la umbo la kibofu cha mkojo.

Kama Unasumbuliwa Na Tatizo Hili Fika Leo Afya Bora Herbal Clinic Iliyopo Njia Panda Ya Kigogo, Karibu na Roundabout kupata tiba na tatizo kutojirudia tena.
0


Inaweza ikawa ndoto yako ni kupata motto wa kiume lakini kila unapojifungua hubahatiki kumpata ukweli ni kwamba kila jambo linapngwa na si kutokea kama miujiza.

Ukweli ni kwamba unaweza mpata motto wa jinsi yoyote unayohitaji iwe wa kiume au au wa kike na hata mapacha.

Inafahamika kwamba watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.

Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.

Leo nitamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…

Kitaalam mbegu zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.

Hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiume XY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..

Usipate taabu tena na kutotimiza malengo au ndoto yako ya muda mrefu, fanya mambo haya ili upate motto wa kiume:-

Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka (ovulation).

Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike na kutengeneza motto (fertilization) hii ni siku ya 14 kabla ya kuona damu ya mwezi unaofuata sio baada ya kuona siku zako..

Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.


Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi ,  siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..

Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..

Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako (sperm count)

Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.

Njia zingine za kuongeza mbegu ni:
Weka korodani kwenye hali ya ubaridi: kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na kuweka laptopkwenye mapaja

Acha kuvuta sigara na kunywa pombe: wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi..

Matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.

Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa (deep penetration)

Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume (XY) kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo (shallow penetration) husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike ( XX).

Hakikisha mwanamke anafika kileleni:


Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.

Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation


Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..kwa maelezo zaidi soma hapa.

Je, Unasumbuliwa Na Matatizo Ya Uzazi Na Haupati Mtoto, Fika Leo Afya Bora Herbal Clinic Iliyopo Njia Panda Ya Kigogo Karibu na Roundabout kupata tiba ya tatizo hilo.
0


Huenda ukawa unataabika kila siku hujapata motto hata mmoja kutokana na kutofahamu kwa namna gani au ni siku ipi ambayo ukishiriki tendo la ndo utapata mimba. Kwani kila hupangwa hakitokei tu kama miujiza.

Siku za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume wake ana matatizo.

Utazijuaje siku hizo?
Kwanza kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako. Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao.

Unajuaje mzunguko wako?
Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata. Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili ue na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadiliki, kama umeshahesabu siku za nyuma kabla ya kusoma makala hii ni vizuri pia. Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu ziko zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je siku za hatari ni zipi?

siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata mimba.

Mfano kama mzunguko wako ni siku wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14. Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa 24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya 14 ni hatari hivyo siku za hatari ni ni siku ya 10,11,12,13,14 na 15.

Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 36 basi chukua 36 toa 14 utapata 22. Hivyo siku ya 22 ni hatari na zingine ni 18,19,20,21,22 na 23.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni hatari kwa huyu mtu.hivyo siku zingine za hatari ni 3,4,5,6,7[mtoto wa kiume] na 8.

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?

Kuongezeka kwa joto kidogo, tumbo kuuma kidogo, na ute mweupe kutoka sehemu za siri..

Maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto. Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano ambazo ndio tarehe yai linashuka ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike.

Fika Leo Afya Bora Herbal Clinic Iliyopo Nji Panda ya Kigogo Karibu na Roundabout Kama Una Tatizo la Ugumba Uweze Kutibiwa na Kupata Mtoto.

0


Degedege Ni Nini?

Ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono, ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili. 

Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa, vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari(hypoglycemia), upungufu wa oxygen(hypoxia), kushuka kwa shinikizo la damu(hypotension) na maambukizi na homa ya degedege.

Homa ni Nini?

Ni hali ya kawaida ya mwili kujikinga na maambukizi. Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi.


Homa ya Degedege Ni Nini?

Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili. Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. 

Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa, niasilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa wa kifafa.

Mmoja kati ya watoto watatu anbao wamewahi kuwa na homa ya degedege wanaweza wakapatwa tena na tatizo hili.baabhi ya watoto wanaweza wasipatwe kabisa na tatizo hili au wakapatwa mara moja tu kwa maisha yao yote. Lakini hauna jinsi ya kutabiri ni mtoto yupi ambaye anaweza kupatwa na shambulio hili.


Homa ya Degedege Hutokea kwa Watoto Gani?


Watoto wanaweza kurithi tabia hii ya kuumwa homa ya degedege kutoka kwa wazazi wao. Kama mama au baba aliwahi kuumwa ugonjwa huu basi mtoto ana asilimia 10-20 zaidi ya kuumwa ugonjwa huu hukilinganisha na yule ambaye wazazi wake hawakuwai kuumwa ugonjwa huu.

Homa isababishwayo na maabukizi yoyote yale kama virus, bakteria na parasite

Dalili za Homa ya Degedege ni Zipi?

Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza mtototo uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili, miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma, baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.

Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni

Macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho

Shambulio huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano
 
Baada ya shambulio mtoto hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima.

Akizinduka anaweza kushindwa hata kukutambua na akawa atamani kitu chochote kwa muda huo.
 
Nini cha Kufanya Mtoto anapopatwa na Shambulio?

Tulia na usichanganyikiwe

Ondoa vitu vya hatari karibu na mtoto na muweke sehemu ya usalama kama sakafuni.

Usijaribu kuweka kitu chochote mdomoni kwa mtoto hata vidole vyako.


Angalia muda wa shambulio kuanza hadi litakapo isha ili umueleze daktari.


Baada ya shambulio kuisha mlaze mtoto kwa upande na usimuamshe muache apumzike.
Shambulio la homa ya degedege sio kifafa na mtoto hapati maumivu yoyote wakati wa shambulio kwa hiyo usimpe dawa yoyote ile.


Baada ya hayo mpeleke mtoto kwenye zahanati, kituo cha afya au hospitali ya karibu kwa matibabu zaidi ya mtoto.



Fika Leo Afya Bora Herba Clinic iliyopo Njia panda ya Kigogo Karibu na Roundabout Kupata Tiba ya Tatizo hili na mengine mengi.
4

Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.

Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.

Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:

Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.

Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani.

Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.

Tikiti pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake. 

Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo. 

Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.

Kwa kawaida tunda hili huliwa peke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.

Huimarisha misuli, Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.

Pia husaidia kupunguza uzito mwilini, Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya

Huimarisha kinga mwili, Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji kina kazi nyingi mwilini, mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Kama unavyojua, kinga ya mwili ndiyo msingi wa afya bora, kwani ukiwa na kinga imara huwezi kusumbuliwa na maradhi hata siku moja.

Huondoa sumu mwilini, ‘Arginine’ vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji madonda na kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

Faida za Tikitimaji kiafya ni nyingi, tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.

Matunda kama haya hupaswa kuliwa mara kwa mara na wakati ungali mzima ili kuupa kinga mwili wako ya kujikinga na maradhi wenyewe, usisubiri mpaka upatwe na maradhi hayo na kwa kuambiwa na daktari ndiyo uanze kula, kumbuka siku zote kinga ni bora kuliko tiba!
0

Friday, August 5, 2016


Ugonjwa wa Kichwa kikubwa ambao kitaalam hujulikana kwa jina la ‘Hydrocephalus’ , huenda ikawa si mgeni kuusikia masikioni mwako.

Jina la ugonjwa huo linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya maji ndani ya kichwa. Ifahamike kwamba sio kila mwenye kichwa kikubwa ana ‘hydrocephalus’.

Kwa kawaida ndani kabisa ya ubongo kuna sehemu nne zenye uwazi, ambazo kitaalam huitwa ‘ventricles’. Sehemu hizo huwa haziko wazi na hivyo kuwa na kiasi fulani ca majimaji yaani ‘fluid’.

Majamaji hayo ambayo jina lake halisi ni ‘Cerebral Spinal Fluid’ hutengenezwa kutoka kwenye damu na chembe chembe (cells) ambazo zipo kwenye kuta hizo za ‘ventrices’.

Majimaji hayo ambayo hutengenezwa ndani kabisa ya ubongo kwenye ‘ventricle’ hupitia sehemu maalum na hivyo kutoka nje ya ubongo na kuuzunguka ubongo na hivyo kufanya ubongo kama vile unaelea kwenye majimaji hayo.

Kwa maana hiyo ndani kabisa ya ubongo kuna ‘ventricles’ ambazo zina hayo maji na kwa nje ubongo umezungukwa na hayo maji.

Ili kuhakikisha maji hayo hayazidi kichwani mwili unao mfumo kamili ambao unahakikisha kuna uwiano kati ya maji yanayotengenezwa na maji ya nayofonzwa na kurudishwa kwenye damu.

Majimaji hayo yanafaida nyingi moja miongoni mwa hizo ni kuweka uwiano wa msukumo (balance intracranial pressure) na kuzuia mtikisiko wa ubongo, (Shock absorber).

Yapo baadhi ya magonjwa ambayo hufanya majimaji hayo yatengezwe kwa wingi kuliko yanavyorudishwa mwilini au maji yanayotengenezwa ni ya kawaida lakini ufyozwaji haupo, na hivyo kuanza kujazana kichwani na kufanya kichwe kiwe kikubwa.

Magonjwa hayo mengi ni yale mtoto anayezaliwa nayo yaani ‘congenital defect’. Pia mtoto anaweza kuzaliwa bila ya shida hiyo lakini akaipata baadae kutokana na kupata magonwa yanayoshambulia zile sehemu zinazofyonza maji hayo.

Magonwa hayo ni kama ‘Meningitis’, ‘Toxoplasmosis’, ‘Cytolomegalovirus’ nk.

Lakini pia kama mtoto atapata baadhi ya kansa ambazo zinashambulia ule utando unaozunguka ubongo (meninges) anaweza pata shida hiyo.

Fika leo Afya Bora Herbal Clinic, ili uweze pata matibabu ya tatizo hili na mengine kadhaa wa kadhaa.
0

Wednesday, August 3, 2016


Mgongo wazi au kwa jina la kitaalam huitwa ‘spina bifida’, ni ugonjwa au hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo ( ule mshipa wa fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi, kutokana na mifupa ( vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.

Kwa kawaida mara tu baada ya mimba kutunga uti wa mgongo hutengewa nusu upande mwingine na nusu upande mwingine.

Baada ya hapo nusu ya mkono wa kulia huunganiswa na nusu ya mkono wa kushoto kama vile mtu anayefunga zip ya nguo.

Ni wakati wa muunganiko huo ndio kasoro inaweza itokee na hivyo sehumu fulani ikawa haijaziba, kama vile ambayo zip ikiharibika inaweza iache katundu mahali.

Sababu zinazofanya kasoro hiyo itokee ni kama kupigwa X ray mama mja mzito, matumizi ya dawa za kifafa, upungufu wa ‘folic acid’, na maambukizi ya baadhi ya virus kwa mama mjamzito.

Shida hii inaweza ikatokea peke yake au pamoja na ‘hydrocephalus’ yaani ugonjwa wa kichwa kikubwa.

Mara nyingi hutokea peke yake lakini baadae ile sehemu iliyowazi hupitisha mambukizi na kusababisha ‘meningitis’, ambayo hushambulia ule utando unaofyonza ‘Cerebral Spina Fluid’ na hivyo kufanya maji yaanze kurundikana kwenye kichwa.
Spina bifida huwapata watoto 3 kila watoto 10000 wanaozaliwa.

Fika leo Afya Bora Herbal Clinic, ili uweze pata matibabu ya tatizo hili na mengine kadhaa wa kadhaa.
0

Tuesday, August 2, 2016


Jambo la kuchagua vyakula sahihi kwa mlo wako inaweza kuwa changamoto na tungependa kuamini kwamba kupungua uzito ni jambo tu la kula kalori chache na kufanya mazoezi zaidi.

Hata hivyo, si mara zote zoezi hili linakuwa rahisi.

Kama ni lengo lako kupunguza uzito, kuchagua chakula gani ule ni muhimu kama kuchagua kiasi gani cha chakula ule.

Ukweli ni kwamba , baadhi ya vyakula vinauwezo wakusaidia kupunguza uzito kutokana na tabia zake za kuunguza mafuta mwilini.
Mafuta ya nazi
Mafuta ya nazi yanapanda chati kwa haraka kabisa na kufanya kuwa mojawapo ya vyakula bora kabisa kwa afya ya binadamu.

Mojawapo ya vitu muhimu kabisa katika mafuta haya ni uwezo wake wa kupunguza uzito wa mwili.

Mafuta ya nazi ni yana kemikali yenye mlolongo wa kati wa mafuta(“Medium Fatty Chain Acids”) ambayo humeng’enywa tofauti na yale yenye mlolongo mrefu wa mafuta(“Long Fatty Chain Acids”)

Kemikali zenye mlolongo mrefu wa mafuta(“Long Fatty Chain Acids”) hupatikana kwa wingi katika vyakula vingi vya mafuta kaa vile nyama,chips n.k.

Kemikali zenye mlolongo wa kati wa mafuta hutumiwa na mwili kwa ajili ya nishati badala ya kuhifadhiwa kama mafuta katika mwili.

Hii ndio sababu mafuta ya nazi ni moja ya vyakula vyenye uwezo wa kuchoma mafuta mwilini na kusaidia kupungua uzito.
Balungi

Balungi yana kiasi kidogo cha kalori , kiwango cha juu cha tindikali za kumeng’enya chakula na inaweza kukufanya usijisikie njaa kwa muda mrefu.

Watafiti wamegundua kwamba kula nusu ya balungi kabla ya mlo ni inachangia sana kupoteza uzito . Pia kula nusu tu ya balungi kabla ya mlo inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha glucose-insulin katika muda wa masaa mawili tu
Kama wewe unahitaji kupungua uzito zingatia kula vyakula vinavyo kata mafuta na ongeza vyakula hivi vilivyotajwa katika mlo wako.

Kwa mafanikio ya muda mrefu , kazania kula vyakula kamili (vyakula visivyo kobolewa au kusindikwa) na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
Siki ya Apple (Apple Cider Vinegar)

Siki ya Apple ina kiwango kikubwa cha kemikali za amino (amino acids) ,kemikali za kumeng’enya chakula na madini na vitamini. Utafiti unaonyesha kwamba kutumia Siki ya Apple kabla ya kula vyakula vya wanga inasaidia kupunguza kupanda kwa insulin hivyo kusaidia kutopata hamu ya kula mara kwa mara.

Ndimu na Limao

Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha vitamini C mwilini kinahusiana na uzito wa mwili.

Watu wenye viwango vya kutosha wa vitamini C wana uwezo wa uwezo wa kuvunja asilimia 30 zaidi ya mafuta wakati wa mwili unapofanya shughuli za nguvu kama kazi za nyumbani,shambani na mazoezi kama kutembea, kuliko wale walio na kiwango cha chini cha vitamini C.

Kama una dhamira ya kupungua uzito, basi fikiria kuanza siku yako kwa kunywa glasi moja ya maji yenye ndimu au limao au anza kutumia siki(vinegar) kwenye kachumbali au saladi unapokula chakula.
0

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.

Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(vyakula vyenye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.
Sababu za kukosa choo:
Kutokunywa Maji ya Kutosha

Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani

Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi

Unywaji wa maziwa kupita kiasi

Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi

Vyakula vinavyosaidia kutibu tatizo la kukusa choo
Tende

Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol–aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.
Maji

Kunywa maji kwa wingi kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.

Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.

Kahawa na Vinywaji vingine vya moto

Kahawa na vinyaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.

Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo

Ulaji wa mboga za majani


Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.

Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.

Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.
Mazoezi pia husaidia kutibu tatizo la kukosa choo

Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.

Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako.

Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).

Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.

Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibi tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.




0

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *