Tuesday, August 2, 2016

Apandikizwa Mbegu Za Mwanaume Mwingine


Huko nchini Marekani katika mji wa Commack, New York, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Nancy Andrew alipata ujauzito usiotokana na mbegu za mumewe baada ya kupandikizwa mbegu za mwanaume mwengine katika kliniki ya upandikizaji (New York Fertility Clinic).

Yeye na mume wake walitegemea kuongezeka kwa mtoto katika familia yao. Walichokuwa hawatarajii ni kupata mtoto mweusi kuliko wazazi wake.

Vipimo vya kutambua vinasaba (DNA Test) vilionesha kuwa madaktari katika kliniki ile walipandikiza mbegu za mwanaume mwengine kwenye mayai ya Nancy Andrew.

Wapenzi hao mpaka sasa wanamlea mtoto huyo waliyempa jina la Jessica kama wa kwao. Hata hivyo, wawili hao wanaona hawakutendewa haki na mwenye kiliniki hiyo pamoja na daktari aliyechanganya mbegu hizo.

Je, ulishawahi kupata majanga yoyoote hospitalini? Tuambie kupitia kisanduku cha maoni au tutumie barua pepe kupitia afyaboraherbalclinic@gmail.com

1 comment:

  1. Casino & Hotel - Mapyro
    Casino 밀양 출장안마 & Hotel. Mapyro is an onsite, fun, and 진주 출장안마 safe location offering fun 영주 출장안마 gaming, 고양 출장안마 dining 사천 출장안마 and accomodations to a select number of US residents.

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *