Monday, August 8, 2016

Huu Ndio Umuhimu Wa Mshubiri au 'Aloe Vera'


Licha ya ladha yake kuwa chungu, mmea wa “Aloe Vera” una faida nyingi kiafya ukitumika kama tiba katika mwili wa binadamu.

Mmea huu umekuwa na majina tofauti tofauti kama ifuatavyo; kwa lugha ya Kiswahili mmea huu huitwa shubiri mwitu, ambapo katika makabila kadhaa mmea huu huitwa majina mbalimbali kulingana na kabila husika.

Wanyaturu huuita ‘mkankiruni’, Wagogo huuita ‘itembwe’ na wahehe huuita ‘Litembwetembwe.’ Mmea huu huwa na umbo linalofanana na mmea wa mkonge au mmea wa mnanasi, ila huu huwa mlaini zaidi.

Majani ya mmea huu yana sehemu mbili, kuna ganda la nje na majimaji ya ndani (jelly). Ganda la nje lina kemikali za kutibu na ule ute wa ndani na lina virutubisho vingi ambavyo husaidia katika kurutubisha kinga za mwili wa binadamu.

Licha ya mmea huu kuwa maarufu duniani kote, umekua ukitumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali kwa binadamu na mifugo.

Mshubiri pori umekua ukitumika pia kwa kutengenezea vipodozi vya aina mbalimbali kwa ajili ya masuala ya urembo. Mmea huu hupatikana sehemu nyingi sana duniani hasa katika nchi zenye joto.

Tafiti zilizofanywa na mtandao wa ‘Mediclinic’ kuhusiana na mmea huu, zinaeleza kuwa mmea huu una uwezo wa kuchochea utengenezwaji wa tishu zenye afya katika mwili wa binadamu.

Imebainika pia kuwa mshubiri huo una uwezo mkubwa wa kufanya mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri na kutuliza matatizo yanayoathiri mfumo wa fahamu.

Mbali na hayo, lakini pia mshubiri “Aloe Vera” ukitumiwa kama tiba husaidia kuondoa sumu mwilini. Mmea huu mara nyingi hutumiwa na kina baba kutibu maradhi ya ngiri (Hernia). Kwa hakika mmea huu una maajabu mengi katika suala zima la tiba.

Naweza nikadiriki kusema, mmea huu ni tunu tuliyotunukiwa wanadamu kutoka kwa Mola wetu kwa ajili ya tiba. Sidhani kama kuna mmea wenye uwezo wa kutibu maradhi mengi namna hii kama ilivyo kwa mshubiri pori.

Haijaishia hapo pia, mshubiri hutumika katika kusaidia kujenga seli mpya katika mwili wa binadamu baada ya kupata majeraha kama vile kujikata, michubuko, majeraha ya moto na hata vidonda vya tumbo.

Aidha, husaidia matatizo ya kutopata haja kubwa, maumivu wakati wa haja kubwa na ndogo na hata husaidia kutibu matatizo ya ngozi na chunusi.

Mshubiri umekuwa ukitumika kwa wagonjwa wenye upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kwa ajili ya kuongeza kinga za mwili (CD4), na imebainika mmea huu unapotumiwa vizuri, mgonjwa wa UKIMWI hujikuta katika hali nzuri.

Watu wengi wamekuwa wakitumia mmea huu kama tiba ya ugonjwa wa malaria, lakini pia mmea huu umekuwa ukichanganywa katika vipodozi mbalimbali ili kuvipa uwezo maradufu wa kutunza ngozi.

Unaweza kutumia mmea huu kwa kukata majani yake na kuyasaga kwa kutumia ‘blender’au kuyatwanga kwenye kinu, na kisha kuyachanganya na maji ya vuguvugu Chuja maji hayo na ongeza maji mpaka upate maji ya kiasi cha jagi moja.

Kunywa vikombe viwili mpaka vitatu kwa siku, kwa muda wa siku tano mpaka saba. Hii itakusaidia kuongeza kinga ya mwili wako na unaweza kurudia dozi hii kila baada ya miezi mitatu mpaka minne.

Ni vema kutumia tiba za mimea ili kuepuka kemikali zisizo za lazima katika miili yetu kiafya. Tukiangalia, pia tunaweza kuona kuwa hata baadhi ya dawa za hospitalini hutengenezwa kwa kutumia mitishamba na mimea ya asili.

Mbali na mmea wa mshubiri kutumika kama tiba kwa binadamu, mmea huu pia unaweza kutumika kama tiba kwa mifugo kama vile kuku. Kwa mfano, ugonjwa wa vidonda vya kuku ambao kwa kitaalam huitwa ‘coccidiosis’ na ugonjwa wa mdondo ambao pia kitaalam hufahamika kama ‘Newcastle disease’ Hutibka kwa kutumia mshubiri.

Baadhi ya watu wamekuwa wakiipanda mimea hii katika bustani za maua majumbani mwao, bila ya kujua umuhimu, faida na maajabu ya mmea huu.

Ningependa kutoa wito kwa Watanzania kutopuuza matumizi ya mmea huu. Ni vema tukautumia kwa ajili ya kinga na tiba za magonjwa mbalimbli katika miili yetu.

5 comments:

  1. Hakika nimejifunza mengi kupitia somo hili japo kuna baadhi nilikuwa nikiyajua lkn mengi nimeongeza katika kuufahamu mmea huu. Ahsante kwa somo zuri.

    ReplyDelete
  2. Nimependa mafunzo yako murua bwana DAKTARI,asante sana Mungu akupe akili ya uvumbuzi wa FIBA zaidi toka kwako miti asilia!

    ReplyDelete
  3. Asante kwa somo maana nilishawahi kutumia kweli na ikatibu, ila nilikuwa nahofu sana kwakuwa niliambiwa nikizidisha nihatari, kwakuwa nimepata somo ninaujasiri, sina shaka tena

    ReplyDelete
  4. Asane nta utumia kwaajili ya kuponya vidonda vya tumbomaana vina nisumbua.
    Je nikiponda na majani yake kisha kuweka maji kuchuja na kunywa haita leta madhara?! Maana nasikia wengine husema ni ule uteute wa ndani tu ndio unachukuliwa.

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *