Tuesday, August 2, 2016

Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi


Katika safu hii ya mapishi, leo tutawaelekeza jinsi ya kupika wali wa nazi.

Wali ni chakula kinachopendwa sana na watu wa pwani hususani wali wa nazi.

Hiki ni chakula kinachopendwa sana na wakubwa na watoto.

Mahitaji :


Mchele kilo 1

Nazi 2 au paketi 2 nazi ya maji

Chumvi kijiko 1 cha chakula

Maji 1/2 lita Jinsi ya kuandaa

Osha mchele vizuri, chuja mchanga.

Bandika sufuria yenye nusu lita ya maji safi.

Yakipata moto, weka nazi yako na chumvi kisha koroga hadi yachemke.

Kisha tumbukiza mchele wako, funika na hakikisha moto si mkali sana.

Subiri kwa dakika 10 kisha ugeuze vizuri wali wako na mara baada ya dakika 20 wali wako utakuwa tayari. Waweza kula kwa mboga yoyote.

Ukifuata maelekezo hapo juu, wali wako utakuwa mtamu na wakuvutia.

Unaweza sindikiza chakula hiki kwa matunda kama embe, ndizi na nanasi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *