Parachichi ni tunda linaloupatia mwili vitamini C. Tunda hili hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Mbeya.
Pamoja na umuhimu wake, tunda hili pia limekuwa likitumiwa na wanawake wengi kama urembo kwa kujipaka usoni na kwenye nywele.
Tunda la parachichi lina faida nyingi kiafya, hususan kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana.
Wanasayansi kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wanaeleza kwamba tunda hilo husaidia katika kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari (free radicals).
Hivyo, linatoa kinga dhidi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana.
Wanasayansi hao wanaeleza kuwa mafuta yanayopatikana katika parachichi yana uwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama ‘mitochondria’.
Kwa mujibu wa wataalam hao, ‘free radicals’ ni kemikali zinazosababisha magonjwa mengi yakiwemo baadhi ya saratani, kuharibu mishipa ya damu ya ateri ‘arteries’, pamoja na kumfanya mtu kuzeeka haraka.
Wanaeleza kuwa mafuta yanayopatikana katika baadhi ya mboga za majani, matunda na nyanya/ tungule yana uwezo wa kupambana na kemikali hizo hatari lakini mafuta haya hushindwa kuingia ndani ya ‘mitochondria’ ambako ndiko kuna kemikali hizo hatari kwa wingi.
Kwa upande wake, mtafiti Christian Cortes-Rojo kutoka chuo kikuu hicho cha Mexico ambaye ndiye alifanya utafiti huo, anasema, ‘anti–oxidants’ zinazopatikana katika mboga za majani na matunda mengi haziwezi kupenya ndani ya ‘mitochondria’, hivyo kushindwa kudhibiti kemikali hatari ndani ya ‘mitochondria’ hizo.
Hatua hiyo huelezwa kusababisha kemikali hizo hatari kuendelea kushambulia ‘mitochondria’ na kuziharibu na matokeo yake ni kuwa nishati haitolewi tena kutoka kwenye ‘mitochondria’ na seli hushindwa kufanya kazi na kufa.
Matokeo ya utafiti huu yalitolewa katika Kongamano la kila Mwaka la Chama cha Wataalamu wa Mambo ya Bayokemia na Bayolojia ya Viumbe Hai kutoka nchini Marekani (American Society of Biochemistry and Molecular Biology Annual Conference).
Kemikali hizi hatari ni uchafu na zinatolewa na mwili wakati wa kusaga chakula na huweza kutolewa kwa wingi kwa mtu anayevuta sigara, mtu anapokumbana na mionzi na hata wakati kukiwa na uchafuzi wa mazingira.
Kemikali hizi huharibu mpangilio wa protini katika muundo wa vinasaba.
Wanasayansi hao wakati wanafanya utafiti waliweza kuona ya kwamba mafuta ya parachichi yaliwezesha seli za ‘yeast’ kuishi kwa muda mrefu kwenye madini chuma licha ya kuwekewa kiwango kikubwa cha madini hayo ambayo ndiyo hutoa kemikali hizi hatari kwa wingi.
Katika tafiti ambazo ziliwahi kufanyika huko nyuma nchini Mexico, ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa parachichi duniani, zilionesha ya kwamba parachichi hupunguza kiwango cha lehemu mwilini na pia hupunguza baadhi ya mafuta yanayohusishwa na ugonjwa wa kisukari.
Mafuta ya parachichi yana virutubisho sawa na mafuta ya ‘olive oil’ yanayohusishwa kwa kusaidia kupunguza lehemu mwilini pamoja na kinga dhidi ya magonjwa mengi sugu kama inavyoonekana kwa watu wanaoishi katika nchi za Mediterania ambao ni watumiaji wazuri wa mafuta haya ya ‘olive’.

Kwa muda mrefu, wanasayansi wamekuwa wakiita parachichi kama mfalme wa matunda kutokana na kuwa na virutubisho vingi kuliko tunda lingine lolote duniani.
Kutokana na umuhimu wa parachichi, kuna haja kwa kila mwanajamii popote alipo kuhakikisha anazingatia somo hili, ikiwamo kulitumia kwa wingi tunda hili kwa manufaa yake.
Pamoja na kila mtu kuhakikisha anatumia tunda hili, ni muhimu pia kwa serikali na hata wakulima kutilia mkazo kilimo cha matunda haya ili kuboresha afya.
Pamoja na kila mtu kuhakikisha anatumia tunda hili, ni muhimu pia kwa serikali na hata wakulima kutilia mkazo kilimo cha matunda haya ili kuboresha afya.
No comments:
Post a Comment