Tuesday, August 2, 2016

Mjue Msichana Anaekupenda


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni ishara zipi au kwa namna gani anaweza kubaini kuwa mwanamke au msihana anampenda.

Hizi ni miongoni mwa ishara zinazoweza kukusaidia kumgundua mkeo au msichana anayekupenda, ila ukumbuke kwamba wanawake au wasichana wanatofautiana ila wengi wao wanalandana.

Mnapoongea;

Wakati mkizungumza haijalishi kuwa ni wapi, sikiliza sauti yake,kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini. anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake na wapo wanaochimba chimba chini.

Mwanake au msichana anaekupenda hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia, huku akitabasamu tabasamu unapoongea nawe kama amekuzoea,ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu.

Anapenda akukumbatie na kukushika;
Unapotembea naye mahali popote anapenda awe karibu nawe akushika mkono wako,au unapokutana naye anaweza kukumbatia. 

Na kama huna tabia hii ni vyema ukawa nayo kwani kumbatio huwafanya watuu wazidi kuwa karibu.

Ajali za kijitakia;

Mwanamke au msichana anayekupenda anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia nakupiga ukelele,au anakukumbatia.anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike,atajitahidi usigundue mbinu zake kwa kupotezea.

Anaibia kukuchunguza;
Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko 'busy' na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.

Watizame marafiki zake;
Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga,hata kama mmeenda 'out' pamoja na marafiki zake utakuta yupo karibu na wewe, akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta,ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe.

Anapenda umjali;

Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

Hawezi kuzuia tabasamu;

Unapomwoneshea tabasamu lazima na yeye arejeshe tabasamu, hata kama kuna kitu kimemuudhi atakuoneshea tabasamu ili mradi aoneshe umemkuta katika hali ya furaha.

Ishara za mwili;
Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini.
kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamuona anashtuka gafla.

Anafurahishwa na vituko vyako
Huwezi ukamboa au kumchosha, hata kama ukifanya kituko ambavyo havichekeshi utakuta anafurahia.

Anakujali;
Anakuwa anakujali,mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza..."unahitaji chochote?....unaweza ukasema " nina kiu ngoja ninunue maji"
utamsikia "nina maji,kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.

ZINGATIA:

Kuna baadhi ya watu wengine wanaweza kufanyiwa hizo ishara zote na wasiweze kugundua, jambo la msingi unatakiwa uwe na muda wa kumsoma mpaka pale atakapokuzoea kabisa na akaanza kushindwa kuficha hisia zake, siyo rahisi kwa wanawake wengi kumwambia mwanaume moja kwa moja kuwa anampenda, baada ya kuona dalili zote unaweza kumtongoza na kumtamkia unampenda utakuwa umemrahisishia kazi.ila kama nawe unampenda.


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI YAKO

Name

Email *

Message *